Nape Nnauye kuzungumza na waandishi Alhamisi hii baada ya kutumbuliwa

Baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli Alhamisi hii kufanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri kwa kumpiga chini aliyekuwa Waziri wa Waziri wa Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo, Mh Nape Nnauye na nafasi yake kuchukuliwa na Dkt. Harrison Mwakyembe, Nape amewataka wananchi kutulia.Nape ambaye alikuwa mstari wa mbele katika tukio la hivi karibuni la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuvamia kituo cha Clouds FM, amesema baadaye atazungumza na waandishi wa habari kuhusu kipigwa kwake chini.
“Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE,” alitweet Waziri Nape.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment