Nay wa Mitego aalikwa Ikulu na Rais Magufuli Ijumaa hii

Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego ameitwa Ikulu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Nay amepata mwaliko huo ikiwa ni sasa chache baada ya kuachiwa huru na Jeshi la Polisi lililokuwa likimshikilia tangu Jumapili.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Nay wa Mitego alikiri kupata mwaliko huo jana na kusema kuwa ameambiwa aende siku ya Ijumaa.
“Yeah ni kweli jana nilipa mwaliko lakini nimeambiwa niende Ijumaa kwa sababu kuna ugeni unakuja kwahiyo na mimi nimealikwa kuhudhuria,” alisema Nay wa Mitego.
Rapa huyo amedai bado nafikiria nini cha kuongea na Rais endapo atapata hiyo nafasi ya kuzungumza naye.
Nay alikamatwa na polisi Jumapili iliyopita mkoani Morogoro na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kutunga wimbo wenye maudhui yanayoikashifu Serikali.
Mapema jana mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema Rais Magufuli ameagiza msanii huyo aachiwe huru na wimbo wake uendelee kuchezwa na kusambazwa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment