Nay wa Mitego adai kukamatwa na polisi Mvomero, ahamishiwa kituo cha kati cha polisi Dar

Nay wa Mitego amedai amekamatwa na polisi wilayani Mvomero, Morogoro alikokuwa ameenda kwaajili ya show.
Hajasema sababu ya kukamatwa kwake lakini watu wanahisi ni kutokana na wimbo wake Wapo ambao umemkosoa vikali Rais Dkt John Magufuli. “Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police,” ameandika rapper huyo mtata.
“Nawapenda Watanzania wote.✊🏿✊🏿 #Truth #Wapo,” ameongeza.
Rapper Nay wa Mitego amehamishiwa katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam kutoka Mvomero, Morogoro alikokuwa ameshikiliwa na polisi kuanzia asubuhi ya Jumapili, March 26.
Taarifa hiyo imetolewa na mwanasheria maaarufu nchini, Peter Kibatala.Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment