P-Funk asimulia jinsi Marco Chali alivyoishia getini Bongo Records alikokuwa akitaka kumuona

P-Funk Majani amewahi kudaiwa kuwa mtu wa mikausho mikali kwa baadhi ya watu hata maarufu, kitu ambacho amesema wakati mwingine hutokana na kuwa na ubusy mwingi kwenye kazi zake.


Producer huyo wa Bongo Records aliwahi kumfanya Marco Chali aishie getini tu katika studio za Bongo Records alikokuwa akitaka kuonana naye ili kujitambulisha na pengine kuomba shavu la kufanya naye kazi.
Haikuwa makusudi, ni kwamba tu kipindi hicho P alikuwa humjui Marco.
“Mfano kama Marco Chali, alikujaga pale akaishia getini. Miaka kadhaa baadaye akaniambia ‘P unajua mimi nilikuja kabla sijaenda kwa Jay au wapi, nilikuwa nimekufuata,” Majani alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.
“Ile unakuta ni ubusy saa zingine, halafu sijapata tu nafasi ya kusikia kipaji chake, lakini labda angenipa demo mwenyewe nisingemkubali kwa kipindi kile, unajua it takes times kuwa bora.”

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment