Picha: Hali ilivyokuwa baada ya waandishi kutangaziwa kuvunjika kwa mkutano wa Nape


 Alhamisi hii mkutano wa aliyekuwa waziri wa habari,utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye ulizuiliwa na jeshi la polisi kufanyika katika ukumbi wa Protea Hotel. Mkutano huo ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na waandishi wa habari ambao walijitokeza katika eneo hilo kwa wingi zaidi kwa ajili ya kufahamu kitakachozungumzwa.
Hata hivyo meneja wa hoteli hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Selemani, alifika katika eneo la mkutano huo na kutangaza kuwa mkutano huo hautakuwepo kutokana na taarifa aliyopewa na RPC wa Kinondoni, Suzana Kaganda.
Hata hivyo nape alifanikiwa kuzungumza na waandishi japo alilazimika kuongea akiwa amesimama juu ya gari nje ya ukumbi huo. Hizi ni baadhi ya picha za waandishi baada ya kutangaziwa kuvunjwa kwa mkutano huo.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment