Polepole: Hakuna mkutano wa Kinana na waandishi wa habari leoKatibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amekanusha taarifa zilizoenea leo asubuhi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Comrade Abdulrahman Kinana atakutana na waandishi wahabari.
Taarifa hiyo ilidai kuwa leo Ijumaa saa nne, Kinana ataongea na waandishi wa habari katika ofisi za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.
“Napenda kukanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kwamba Katibu Mkuu wa CCM Komrade Kinana atakuwa na Mkutano na waandishi leo. Asante,” ameandika Polepole kwenye Twitter.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment