Rais Magufuli awaonya wamiliki wa vyombo vya habari ‘hamna uhuru wa kiasi hicho, kuweni makini’

Rais Dkt John Magufuli amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu wanavyotumia uhuru wao kupitiliza na kwamba wajiangalie

Rais ametoa onyo hilo leo wakati akizungumza ikulu katika hafla ya kuwaapisha mawaziri wapya wawili aliowateua akiwemo Dkt Harrison Mwakyembe anayechukua nafasi ya Nape Nnauye katika wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo.
Amemtaka Dkt Mwakyembe kwenda kufanya kazi na kuchukua hatua stahiki huku akioneshwa kukerwa na jinsi vyombo vya habari vilivyolipa uzito suala la askari aliyemtishia bunduki mheshimiwa Nape.
“Hatuwezi tukaiacha serikali ikaangamia sababu ya watu wachache haitawezekana. Hata kasomeni tu hayo magazeti ya leo picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba hicho kitendo kimefanywa na serikali au kinasapotiwa na serikali, page ya kwanza, page ya pili, huyu anatoa anafanya hivi, huyu anafanya hivi that’s the story,” amesema Rais.
“Nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari be careful and watch it. Kama mnafikiri mna freedom ya namna hiyo not to that extent,” alionya.
“Watu wanasema habari za huyu zimezuiliwa, lakini unakuta habari za kumtukana zimechapishwa tena, sasa kama zimezuiliwa si hata za kumtukana msiziandike!”
Rais Magufuli ameviasa vyombo vya habari kupendelea kuandika habari za maendeleo na sio zile zenye asili ya uchochezi.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment