Siwezi kubishana na TID ambaye akiona gari yangu analikimbia apate chochote kitu – Steve Nyerere

Baada ya msanii wa filamu za vichekesho Steve Nyerere kuambiwa yeye ni panya na TID, muigizaji huyo ameibuka na kujibu mapigo.

Wawili hao walianza kutupia maneno kutokana na sakata la madawa za kulevya baada ya muigizaji huyo kudai TID alilipwa milioni 2 na RC Makonda kuzungumza mbele wa waandishi wa habari kuhusu issue ya yeye kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
Muigizaji huyo alidai yeye hawezi kuanza kujibishana na TID kwa kuwa TID si kitu chochote.
“Siwezi kubishana na TID ambaye akiona gari yangu analikimbia apate chochote kitu. Kwahiyo nikianza kubishana naye nitakuwa napoteza muda, halafu mimi na TID ni kama vidole kuna kikubwa na kidogo yeye wakati wake ulishapita huu ni wakati wa Steve lazima ajenge heshima,” Steve Nyerere alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Aliongeza “Alivyonifananisha na panya nimependa kweli, kwanza namsifu kwa sababu amenifananisha na kiumbe mjanja. Kwahiyo mimi nasema bora mimi panya kuliko yeye paka ambaye anasubiri atengewe ale, nimefurahi sana kwa sababu amenisifia kunifanisha na mnyama mjaja,”.
Kuhusu issue na kuburuzwa mahakamani kwa tuhumu alizozitoa dhidi ya TID, Steve Nyerere ameomba radhi kwa kauli ile huku akidai tayari alishaomba msahama mbele ya waandishi wa habari kwa wote aliowazungumzia kwenye audio ambayo ilisambaa mitandaoni.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment