Ukiletwa ushahidi nina uhusiano na msanii najiuzulu uwaziri – Nape

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema atajiuzulu uwaziri endapo mtu atampelekea ushahidi wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote.

Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV, Nape alieleza kushangazwa na kitendo cha kuhusishwa kuwa na mahusiano na wasanii.
“Ni katika watu kukosa hoja ila kama mtu ana ushahidi alete hapa mezani asema Nape eeh ili unalolifanya unalifanya kwasababu una mahusiano na mtu alete na ushahidi akileta mimi najiuzulu uwaziri,” alisema.
“Hii ni katika watu ambao wanakosa hoja halafu wanasingizia hoja ambazo hazina msingi, ningefurahi mtu akisema Nape hana sababu ya kutumia busara, twende na hoja hii nyingine ni upuuzi,” aliongeza.
Akizungumzia kuhusu kutajwa kuhusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasanii, Nape alisema wasanii wengi ni wadogo zake akiwemo Wema.
“Majority ya hawa ni wadogo zangu. Wamezungumza habari ya Wema, sasa nieleze ukweli kwamba baba yake, Mzee Sepetu (Isack) na baba yangu (Moses Nnauye) ni mtu na kaka yake, kwahiyo Wema ni mdogo wangu sana sana. Mama yake anatoka Singida, mama yangu naye anatoka Singida, ni mtoto mdogo lakini mtu akiamua apoteze ‘direction’ (mwelekeo) ya mjadala anaweza kuja na hoja nyingi sana.”
“Mimi nimeanza kufanya kazi na wasanii, nimefanya nao kazi kwa miaka 16 sasa, hii ya uwaziri imekuja juzi tu. Pia msisahau hawa wasanii tuliwatumia kwenye kampemi ya CCM, mimi ndiyo nilikuwa Katibu wa Uenezi wa CCM. Ukizungumza burudani, hamasa na ‘publicity’ mimi ndio nashughulika nayo, hivyo kuwaingiza wasanii kwenye kampeni haikuwa kazi rahisi, sasa nikiwa nao karibu dhambi inatoka wapi, maana ndio nilipewa dhamana ya kuwasaidia. Hizi hoja zingine ni za kijinga kabisa,” alisema Nape.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment