Vanessa Mdee apata baraka za Mchungaji Gwajima

#FreeVanessaMdee haijaishia kutrend kwenye midomo ya mashabiki na wasanii pamoja na kwenye mitandao ya kijamii peke yake, weekend hii.


Vee Money ameonekana kuwa special katika mastaa wote waliohusishwa na skendo ya madawa ya kulevya baada ya umma kuonesha kumtetea kwa nguvu zote. Muimbaji huyo pia amepata baraka toka kwa Mchungaji Gwajima ambaye tangu naye ahusishwe na biashara hiyo amekuwa akifurumisha series za mabomu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza mbele ya waumini wa kanisa lake, Gwajima alisema:
Sasa hapo ndio najiuliza, polisi na uhamiaji waseme kwanini wanasuasua na kuna makosa niliyoyataja angalau saba ya jinai wakati wengine wamelala ndani kwa kuhisiwa tu wakiwemo wanamuziki kwa mfano Vanessa Mdee, amelala ndani tu alikuwa nje wakati sisi ametajwa naye ametajwa amerudi ndani leo siku ya tatu Vanessa Mdee leo yuko ndani kwa kuhisiwa tu, lakini huyu mpaka tumetaja Daudi Bashite yupo katorokaje? Huyu kakimbiaje? Vanessa Mdee simfahamu wala simjui lakini alikuwa ana performing zake nje ya nchi kashikwa pale yuko ndani leo, huyu katorokaje? Kwanini wengine wako ndani na wengine wanazunguka mitaa ya South Africa wakati walitakiwa wawe hapa na wao, mbona mimi nilienda kulala tu?
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.