Anna Mghwira -Tanzania haina uchaguzi wa demokrasia

Aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama cha siasa ACT – Wazalendo, Anna Mghwira amedai Tanzania bado haina uchaguzi wa demokrasia huku akiweka wazi mpango wake wa kugombea ubunge katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020 jimbo la Singida.

Mwanamama huyo ambaye alionyesha ujasiri mkubwa katika mbio za kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2015, amesema hayo Jumatatu hii wakati akizungumza kupitia kipindi Cha Dakika 45 cha ITV.
“Siwazi siioni Tanzania ya uchaguzi ya mwaka 2020. Hatuna chaguzi za demokrasia bado. Pengine naweza kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Singida mjini mwaka 2020,” alijibu Mama Anna Mghwira wakati akieleza mipango yake katika uchaguzi ujao.
Katika hatua nyingine Mama Anna aliishauri serikali kuwekeza katika kilimo ili kuiandaa Tanzania ya Viwanda.
“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda bila ya kuboresha kilimo kwanza, Tunahitaji kuwa na Tanzania ya kilimo kwanza,” alimema.
by Yasin Ngitu

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment