Ben Pol na Songa waibuka washindi kwenye tuzo za Mdundo

Kwa mara ya kwanza, kampuni ya muziki ya Mdundo.com inayowezesha mashabiki kupakua nyimbo mbalimbali za wasanii wa muziki hapa nchini Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla, Ijumaa hii, Machi 31, 2017 imefanikiwa kutoa tuzo kwa wasanii ambao wameshinda kutokana na wingi wa upakuaji wa nyimbo zao.


Kutoka Kushoto: Meneja wa Songa, Chin, Songa, Sintah (Mdundo Tanzania), Tiddy Hotter na Prisna Nicholaus (Mdundo Tanzania)
Katika tuzo hizo wasanii waliopata ushindi ni pamoja na Ben Pol ambaye amefanikiwa kuchukua tuzo mbili, Msanii wa bora wa Afropop pamoja na wimbo bora uliopakuliwa zaidi, huku tuzo ya msanii bora wa hiphop ikichukuliwa na Songa. Washindi hao walipata nafasi ya kujumuika pamoja na kupata chakula cha mchana katika maeneo ya Masaki kwenye kiota cha Alcove Restaurant.
Tuzo hizo ambazo zilikuwa zinawaniwa na wasanii mbalimbali, zilikuwa kwenye vipengele vikuu vitatu:
Kipengele cha wimbo ulio pakuliwa zaidi:
Washiriki:
1: Enzi Za Utoto – Songa
2: Forever – Ruby
3: Juu – Jux and Vanessa
4: Kamatia – Navy Kenzo
5: Mahaba Niue – Maua Sama
6: Moyo Mashine – Ben Pol
7: Siwezi – Braka Da Prince
8: Skendo – Mo Music
9: Uzuri Wako – Jux
Kipengele cha Msanii bora wa Hip Hop:
1: Chindo Man
2: Dizasta
3: Gnako
4: Godzilla
5: Nikki Mbishi
6: One The Incredible
7: P The Mc
8: Songa
9: Young Killer
Kipengele cha Msanii Bora wa Afropop:
Washiriki:
1: Barakah Da Prince
2: Belle 9
3: Ben Pol
4: Christian Bella
5: Jux
6: Maua Sama
7: Mo Music
8: Navy Kenzo
9: Ruby
10: Vanessa
Unaweza ukatazama hapa picha za tuzo hizo:
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment