Diamond adai hali ya muziki sio shwari, amshauri Shetta kufanya ‘muzikisiasa’ lakini…

Msanii wa muziki Diamond Platnumz amefunguka kwa kudai kuwa hali ya muziki sio nzuri huku akimshauri muimbaji Shetta kufanya nyimbo ambazo ndani yake zina masuala ya siasa kutokana hali ya muziki utawaliwa na siasa.


Muimbaji huyo wiki iliyopita aliachia wimbo ‘Acha Nikae Kimya’ ambao ulimletea matatizo makubwa katika mitandao ya kijamii hali iliyomfanya aombe radhi.
Jumapili hii muimbaji huyo amerudi tena kwa kumshauri Shetta kufanya muziki huo huku akimtaadharisha kwa mambo mawili.
“Shetta ndugu yangu, Najua unanionea gere mwenzako toka juzi insta imehamia Madale….na wewe unataka kuingia kwenye huu upepo wa #Mzikisiasa …we usijiulize ingia tu😁…maana mjini sasa hivi vingoma vya Mapenzi Vigumu…ikiwezekana jifanye hata unataka kumtolea Mahali Mange Umuoe…Kesho mji wote wako…..ila kuna mawili: Sentro au Matusi😅😅😅😅 – #SimbaMason,” aliandika Diamond Instagram.
Wasanii wengi hivi karibuni wamekuwa wakilalamika kwamba wanashindwa kuachia project zao mpya kutokana na matukio mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment