Harmonize hawezi nipiga chini – Wolper

Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amefunguka kwa kudai kuwa mpenzi wake wa sasa Harmonaze hana uwezo wa kumuacha kimapenzi pamoja na tetesi ambazo zimekuwa zikisikika kwamba mwanamuziki huyo kuwa ana warembo wengine anaotoka nao kimapenzi.


Wawili hao kwa sasa wako karibu zaidi baada ya wiki chache zilizopita kudaiwa wameachana.
Akiongea na mtandao wa Central Filamu wiki hii, Wolper amedai yeye na Harmonize wako vizuri na hawadhani kama wenaweza kutengena hivi karibuni.
“Wengi wanaongea sana kuhusu mpenzi wangu kama anatoka na wanawake wengi pengine inaweza kuwa ndio sababu ya kuniacha mimi hicho hakiwezekana wanaongea kama kuna wasichana wanajipendekeza watachezewa tu,” alisema Wolper.
Muigizaji huyo amedai Harmonaze hana uwezo wa kumwacha kwani yeye ni muhimu kwake.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment