JB atangaza msimamo mpya kuhusu filamu ‘feki’ za nje

Msanii mkongwe wa filamu, Jacob Stephan ‘JB’ amedai kama serikali itashindwa kuzuia filamu ‘feki’ za nje ambazo hazilipi kodi na wao watagoma kulipa kodi.

Muigizaji huyo alikuwa ni mmoja kati ya wasanii wa filamu alioandamana kuitaka serikali kuzuia filamu ‘feki’ za nje ambazo hazilipi kodi.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, JB amedai wao kama wasanii, serikali ikishindwa kuwadhibiti wafanyabiashara wa filamu ‘feki’ za nje na wao hawatalipa kodi.
“Sisi kama wasanii tunaimani na serikali yetu, ni serikali makini na sikivu na tunajua hili suala litashughulikiwa tu,” alisema JB.
Aliongeza,“Nia yetu walipe kodi kama sisi, kama wakiendelea kufanya biashara bila kulipa kodi na sisi tutagoma kulipa kodi kwa sababu wao wanauza bidhaa zao kwa bei nafuu kwa sababu hawalipi kodi,”
Katika hatua nyingine muigizaji huyo alidai wale wasanii wanaopinga juhudi zao ni waigizaji ambao wako kwenye tasnia lakini wanafanya kazi nyingine nje ya filamu.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment