Lulu akana taarifa kuhusu Ndoa

Muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) akana kutoa taarifa za ndoa yake.


Hivi karibuni magazeti ya Mtanzania na Mwananchi yaliobnekana kufanya mahojiano na mrembo huyo na kuripoti kuwa ndoa yake na mpenzi wake Fransic Shiza maarufu kama Majay ambaye pia ni bosi wa EFM na TVE inakaribia.
Kupitia mtandao wa Twitter, Lulu amekanusha taarifa hizo kwa kuandika, “Hivi kwa Akili yenu Ndoa inatangazwaga Kwenye Magazeti!??Muwege mnajiongeza kabla ya kuparamia Story…!.”
Kwenye gazeti la Mtanzania la siku chache zilizopita, lilinukuu kauli ya muigizaji huyo aliyosema, “Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment