Mabaga Fresh wageuka kuwa madereva wa Bajaji

Kama unatumia sana usafiri wa Bajaji, siku moja unaweza ukawa na bahati ya kupelekwa uendako na Mabaga Fresh


Wasanii hao waliowahi kutamba kitambo na wimbo Tunataabika, wamegeuka kuwa madereva wa Bajaji.
“Tumekaa kimya sana kwenye muziki kwasababu tulibadilisha fani baada ya kuona kwenye muziki mambo yanatuvuruga tukaamua mimi hapa Dj Snox na mwenzangu JB mkuu wa Majaji kuingia kwenye kazi mpya ya kuendesha bajaji ili kujitafutia chochote kitu,” amesema Snox kwenye kipindi VMic cha Channel Ten.
“Na kazi hio ndio tunaifanya mpaka leo hii na kituo chetu cha Bajaji kipo Kariakoo Gerezani pale mwisho wa magari ya mwendokasi,” aliongeza.
Kwa sasa Mabaga Fresh wana nyimbo mbili mpya, moja ni singeli inaitwa MAISHA YA MTAA wamemshirikisha DOGO NIGA na wimbo mwingine unaitwa KIDAWA ambao ndani yake wamemshirikisha Q-CHILLA.
Nyimbo zote zimefanyika kwa producer D ambaye ndio kama meneja wao kwa sasa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.