Mamia wajitokeza kumzika baba yake Belle 9, Morogoro

Mastaa wa muziki pamoja na wadau mbalimbali wamejitokeza kwa wingi hapo jana katika mazishi ya baba wa staa wa muziki, Belle 9 aliyefariki akiwa hospitalini mkoani humo usiku wa Machi 18 akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na pikipiki.

Belle akiwa na wasanii pamoja na wadau mbalimbali mbele ya kaburi la marehemu baba yake baada ya mazishi.
Meneja wake, Jahz Zamba, aliiambia Bongo5 kuwa Mzee Damian amefariki dunia baada ya kugongwa na boda boda iliyokuwa kwenye mwendo mkali huko mjini Morogoro alikokuwa anaishi.
Alivunja mguu mmoja pale pale na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupelekwa hospitali. Dereva wa boda boda naye aliumia vibaya ikiwemo kuvunjika taya na kujeruhiwa kichwa.
Jahz alisema baada ya Mzee Damian kupelekwa hospitali na kuwekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahtuti, kuna dawa zilikuwa zikihitajika lakini zilikosekana kwenye hospitali hiyo. Amesema kaka yake Belle anayeishi Morogoro aliingia mtaani kuzisaka na aliporudi mida ya saa sita usiku alikuta Mzee ameshafariki.

Ni pengo kubwa kwa Belle 9 kumpoteza baba yake kwakuwa mara nyingi hudai baba yake ni mwalimu muhimu katika maisha yake. Muimbaji huyo anayetokea Morogoro alimtaja mzazi wake huyo kuwa ni mtu anayemuinspire kwa mengi.
Tunampa pole Belle kwa msiba huo mzito na Mungu ailaze roho ya baba yake mahala pema peponi.
Mtayarishaji wa muziki, Mona (kushoto) akiwa Morogoro.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment