Miaka 5 baada ya kifo cha Kanumba, mama yake ameyasema haya

Leo April 7, 2017 imepita miaka mitano tangu muigizaji nyota Steven Kanumba ‘The Great’ afariki dunia ambapo mama mzazi wa staa huyo Bi. Flora Mtegoa ameshangazwa na wasanii wa Bongo movies.

Kupitia Clouds TV Bi. Mtegoa amedai kukimbiwa na marafiki wengi baada ya Kanumba kufariki April 7, 2012 na hata wasanii ambao walikuwa karibu yake kipindi cha uhai wa mwanawe hawaoni tena siku hizi.
“Baada ya kuondoka Kanumba, mimi kwangu mpweke na imenipunguzia marafiki maana kulikuwa na marafiki waliokuwa wananipenda mimi kupitia yeye ila nashukuru wengine wapo ambao hata leo nilikuwa nao makaburini.
“Unajua mti ukidongoka matawi yanaangaika, lakini sasa hivi nimeshajikusanya, nimesimama maana niliyumba kimawazo, lakini nashukuru kazi yake ya mwisho ilivyotoka fedha zilitoka na nililipwa fedha zangu.
“Nam-misi Kanumba, pili ule ushirikiano wa wasanii wa Bongo movie siuoni na wale waliokuwa marafiki sana wa Kanumba siwaoni makaburini. Baada ya kuzika na sielewi ni nini maana mtu ameshafariki na bado unamuwekea kinyongo? Na nasema tumkumbuke kwa mema japo nashukuru kwa wale waliofika makaburini japo ‘Umimi na Ubinafsi’ ndiyo unaoharibu Bongo Movie.” – Bi. Flora Mtegoa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment