Mr Blue aeleza kwanini anasita kuachia ngoma mpya

Tangu ngoma yake Mboga Saba aliyomshirikisha Alikiba itoke, Mr Blue ameonekana kuchukua mapumziko marefu bila kuachia nyingine.


Na sasa ameeleza sababu za kukaa kimya. “Sijaachia wimbo mpya hadi hivi sasa kwasababu mimi huwa nawasikiliza mashabiki zangu, wakiniambia nitoe natoa hata leo,” Blue alikiambia kipindi cha VMix cha Channel Ten.
“Na kwa kipindi ambacho nimekaa kimya mashabiki zangu wengi wananiambia niache kuimba, eti blue kuimba waachie watoto wadogo wewe rap tu, aah kwakweli bado nawafikiria kwa sababu mashabiki zangu ndio kila kitu kwangu,” aliongeza.
“Mpaka sasa nina nyimbo mbili ambazo ziko tayari na muda wowote naachia moja wapo.”
Imeandikwa na Nelson Munema (Mtangazaji, VMix – Channel Ten)
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment