RC Makonda atembelea miradi 2 itayozinduliwa Leo Jumamosi na Rais Magufuli

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekagua mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na mradi ya nyumba za wananchi Magomeni (Magomeni Kota).

RC akizungumza na waandishi wa habari.
Miradi hiyo miwili itazinduliwa Jumamosi hii na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Akiongea na waandishi mapema leo, RC Paul Makonda alisema hosteli hizo ambazo zimegharimu shilingi bilioni 10 zitakuwa na uwezo wa kumudu zaidi ya wanafunzi 3,840.
“Hizi zitakuwa hosteli za wananchi wa chini kabisa kama ambavyo Rais wetu amekuwa akieleza nia yake ya kuwasaidia wananchi wa chini, hapa kila mmoja atakuwa akilipa shilingi laki moja na elfu kumi tu kwa muhula mzima, hicho ni kiwango cha chini ukulinganisha na kodi za hosteli zilizopo mitaani,” alisema RC Makonda.
Katika hatua nyingine RC Makonda amearifu kuwa kesho mara baada ya Uzunduzi huo, Rais Magufuli pia ataweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa nyumba za Magomeni kota sambamba na uzinduzi wa mtambo wa kuandalia Zege.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment