Spika Ndugai aagiza polisi kumkamata Halima Mdee

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kwa tuhuma za kutumia lugha za matusi.


Spika Ndugai ameagiza mbunge huyo kukamatwa akiwa bungeni mjini Dodoma.
“Kwahiyo Halima Mdee popote alipo katika nchi hii, najua hayupo Dodoma by saa hii awe yeye mwenyewe awe amejileta bungeni. La sivyo akamatwe na polisi popote pale alipo aletwe kwa pingu hapa bungeni hatuwezi kucheza katika mambo ya msingi, tuelewane kabisa tumekuja mmoja mmoja hapa,” amesema Spika Ndugai
Mbunge huyo alitoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment