Tunda aeleza jinsi sakata la dawa za kulevya lilivyobadili maisha yake

Video queen Tunda amedai kutajwa kwake kwenye orodha ya wanaohusika na dawa za kulevya kumempa changamoto ya kuaminika nyumbani kwa wazazi wake.


Mrembo huyo amekiambia kipindi cha Enewz cha EATV kuwa tangu kutajwe kwenye wahusika wa matumizi ya madawa imemfanya kubadilisha mfumo wa maisha kwa kuwa nyumbani kwa wazazi wake wamekuwa wagumu kumuelewa.
“Nimebadilisha mfumo wa maisha, naishi maisha ya low profile kwa sasa ili mambo kwanza yatulie lakini nipo. Maisha ya mitandaoni nimeacha. Suala la kutajwa linaniumiza kwa sababu nyumbani haikuwa rahisi kueleweka na wazazi,” alisema Tunda.
Aliongeza, “Viongozi wanadai natumia mimi ndo niseme najitetea ukweli ni vigumu mno lakini naamini kwenye ukweli uongo hujitenga pembeni ipo siku ukweli utajulikana na maisha yataendelea kama kawaida. Niweke wazi situmii madawa ya kulevya.”
Tunda na baadhi ya mastaa wengine wapo nje kwa dhamana baada ya kutuhumiwa kuhusika na matumizi ya madawa ya kulevya.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment