Vanessa Mdee ashirikishwa na producer wa nyimbo 2 kwenye album ya Beyonce (Lemonade) Diplo (Major Lazer)

Vanessa Mdee anaendelea kwenda Juu. Fresh kutoka kutumbuiza kwenye tamasha la muziki la Gidi jijini Lagos, Nigeria wikiendi ya Pasaka, Cash Madame huyo ameonekana kuingia location kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na kundi la watayarishaji wa muziki, Major Lazer linaloongozwa na Dj wa Marekani, Diplo.
Vanessa Mdee akiwa na Diplo
Kwenye wimbo huo pia member wa Major Lazer, Mmarekani mwenye asili ya Jamaica, Walshy Fire ameshiriki na kuufanya kuwa mradi wa Major Lazer ft. Vanessa. Diplo na Walshy Fire nao walitumbuiza kwenye tamasha la Gidi.
Vanessa na Walshy Fire
Vanessa ameshare picha kwenye Instagram akiwa location na watayarishaji hao na kuandika, WORLDWIDE πŸŒŠπŸ‡―πŸ‡² x πŸ‡ΉπŸ‡Ώ x πŸ‡ΊπŸ‡Έ @diplo @walshyfire Happy Easter πŸ˜˜ #MajorLazer #VeeMoneyIfYouNasty.”


Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment