Wema Sepetu amchana Harmorapa, ‘Usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa’

Harmorapa ameingia choo cha kike. Wema Sepetu amemjibu rapper huyo asiyeishiwa vituko juu ya ujumbe wake aliouandika wiki iliyopita kwenye mtandao wa Instagram kuwa akifanikiwa kumpata mrembo huyo atatangaza ndoa na kumtimizia kila anachokihitaji.

Kupitia mtandao huo huo, Wema ameonekana kukasirishwa na ujumbe huo na kuamua kumuandikia barua yenye ujumbe mzito chipukizi huyo anayekuja kwa kasi.
Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo. Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa ktk chama changu CHADEMA, usiniharibie kwenye familia yangu, marafiki zangu na usiniharibie kwa niliye nae. Ni utoto na ujinga kuposti kila uchao picha za wanawake eti wanakutaka au unatoka nao *DO U THINK NAMI NI WA AINA HIYO?* Usidharaulishe. Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one but *AM NOT FOR U* and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako *LETS STOP THERE*
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment