Albert Msando aomba radhi baada ya video yake chafu na Gigy Money kusambaa

Mwanasheria Albert Msando amewaomba radhi ndugu, jamaa pamoja na mashabiki baada ya kusambaa kwa video yake mtandaoni inayomuonyesha akishikana na video queen, Gigy Money.


Msando akiwa katika shughuli zake
Msando amesema anawaomba msamaha wote aliowakwaza, wote walio kereka na video hiyo ambayo alipokelewa vibaya na mashabiki wengi mtandaoni.
“Nikikaa kimya nitakua mnafiki. Nimekosea. Kilichotokea hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is we all are human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu. Ni sawa na ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats friendship. #TheDon #Hennessy #TheClip” aliandika Msando kupitia Instagram.

Picha ya sehemu ya video hiyo ikiwaonyesha wawili hao
Mashabiki katika mitandao ya kijamii wamemshangaa mwanasheria huyo kutoka na hadhi yake.
Hata hivyo Msando hakuweka wazi ni nani aliyevujisha video hiyo mtandaoni.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment