BASATA yaridhia zawadi ya gari aliyopewa Miss Tz Diana

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) wamesema wameshuhudia Alhamisi hii Miss Tanzania 2016/17 Diana Edward akikabidhiwa zawadi ya gari aina ya Suzuki Swift kutoka kwa kamati ya Miss Tanzania.Gari aliyokabidhiwa Miss Tanzania
Zawadi hiyo amekabidhiwa ikiwa ni miezi sita toka atangazwe mshindi baada ya aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuingilia kati sakata hilo na kutoa agizo kwa kamati ya Miss Tanzania kumkadhi mrembo huyo zawadi zake kama alivyoahidiwa.

Akiongea na Bongo5 mwakilishi wa BASATA muda mchache baada ya kushuhudia makabidhiano hayo, Kelvin Makame alisema yeye alitumwa na baraza hiyo kushuhudia kama ni kweli miss huyo anakabidhiwa zawadi ya gari ambayo aliahidiwa.
“Mimi hapa nilikuja kushuhudia kama kweli kamati ya miss Tanzania inamkabidhi mshindi zawadi yake. Gari nimeliona na tayari amekabidhiwa la zamani au jipya mimi sijui tayari kuna kamati ya tathini ambayo iliunda na kwenda kuliangalia baada ya kurithika nalo ndio wakaamua kumkabidhi, na yeye mwenyewe amelikubali,” alisema Makame.
Makame amedai Miss Tanzania amechelewa kukabidhiwa zawadi hiyo kutokana na wadhamini wa mashindano hayo kuchelewa kukabidhi zawadi kwa kamati ya Miss Tanzania.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment