Ben Pol anena haya baada ya picha zake za utupu kuwa gumzo

Ben Pol amefunguka kwa mara ya kwanza tangu picha yake inayomuonyesha akiwa utupu kusababisha maneno mengi mitandaoni.


Muimbaji huyo amerudi tena kupitia mtandao wa Instagram kwa kuweka video ambayo inamuonyesha akiwa mtupu huku ukisikika wimbo ukiimba na kuandika, “Usi-judge kitabu kama hujakisoma ndani 🤔.”
Hata hivyo imeonyesha kuwa picha hizo zilizozua utata mkubwa mapema wiki hii ni ujio wa nyimbo yake mpya ya Ben ambayo imedaiwa kupewa jina la ‘Mateka’ na ndani yake amemshirikisha rapper Darassa.
Wimbo huo pia umetayarishwa na Tiddy Hotter ambaye alitengeneza wimbo mwingine wa Phone wa Ben.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment