Common amtetea Kanye west

Msanii wa Marekani Common, amemtetea msanii mwenziye Kanye West, kutokana na hatua aliyoichukua ya kuamua kukaa mbali na watu na kuamua kwenda kuishi katika milima kwa ajili ya kutengeneza album yake.


Common ambaye naye ni rapa anayeishi Los Angeles, amesema kuwa anaamini Kanye ataweza kutengeneza album kali na nzuri hivyo ni sahihi kwake kufanya kile ambacho anahitaji kufanya.

Common, Kanye West
Safari ya Kanye inatajwa kuwa ilifanyika wiki mbili zilizopita ambapo alielekea kwenye milima inayopatikana mji wa Wyoming magharibi mwa Marekani.
”Ni muhimu kwa msanii kama Kanye kutafuta sehemu yenye furaha na kuhakikisha anaandaa albamu bora kwa ajili ya mashabiki” amesema Common.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment