Gigy Money: Wema Sepetu ni mwanamke feki (Video)

Gigy Money ameendelea kuchafua hali ya hewa na safari hii amemchana Tanzanian sweetheart Wema Sepetu kuwa ni feki.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Gigy amedai japo mwanzoni alitamani sana kuwa kama Wema na kukiri kuwa muigizaji huyo alishawahi kuwa role model wake lakini kwa sasa hataki tena anamuona anaishi maisha ya kuigiza.

“Wema ni mtu ambaye she is fake, Yaah! She is fake. Ukimuona WQema hivi live na ukimuona mtandaoni unaweza ukavurugwa, watu wengi ambao hawajawahi kumuona Wema hivi live wanachanganyikiwa, sio kama mimi sasa hivi. Mimi nilikuwa navurugwa magazeti kila siku nikiensda shule napitia Wema kafanya nini? Sasa hivi naishi hayo maisha sasa huwezi kuniambia Wema she is real,” alisema Gigy.
“Mimi naishi hayo maisha by real sasa ndio maana kwake inakuwa changamoto, atafanya nini. Mimi ni changamoto kubwa sana kwa kila mtu ambaye yupo kwenye industry hii, maana sasa hivi unaweza ukaenda kwenye interview ukamfanyia msichana anayekuja interview akamtaja Gigy from nowhere pia. Mimi sifanyi kwaajili nashindana, nafanya kwa ajili yangu,” ameongeza.
Model huyo wa video za muziki, amesisitiza kwa kusema, “Mimi ukweli zamani nilikuwa natamani kuwa kwenye Bongo Movie niwe kama Wema Sepetu, nilikuwa naamini Wema ni msichana mzuri hakuna, nilikuwa naona kukaa hata na Wema na mimi ninaweza nikawa hata mtu kumbe wee! No, mimi ni Gigy Money na watu watataka kuwa Gigy Money soon. Kila mtu ana brand yake na ana nyota yake, usitamani kitu cha mtu, Yule ni Wema hamuwezi kumpambanisha na mtu yoyote.”
Gigy ameendelea kwa kuwataka mashabiki wampe nafasi na vyeo vyake ili awe top na wamthamini kama wanavyofanya kwa madam Sepenga. Akiendelea kufunguka kuhusu Sepetu Gigy amesema, “Last time nimekutana naye hawezi kupiga stori na mimi tena, nimekutana naye kwenye birthday ya Sallam, nilicheza sana lakini nilikuwa ba bae Dangote.”
“Alinuna kweli na alikuwa ananiangalia vibaya lakini unajua ni mtu ambaye alishakuwa inspiration kwangu kwa hiyo siwezi kuonyesha action yoyote kwangu na kiukweli am the first person nilimwambia umependeza, wakati anaingia, am real. Ni kweli alivaa kizamani na umbo lake lilivyokubwa mashallah, alipendeza lakini nilivyopingia ndani tena sasa nilivyoitwa na Dangote kisa kuna Wema tena, niacheni kidogo siwezi kuvumilia. Sasa nikawa nacheza mimi na Dangote akawa ananiangalia mimi,” ameendelea.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.