Harmorapa afunguka kuhusu kuvaa gauni

Harmorapa amefunguka kuhusu video inayosambaa mitandaoni ikimuonyesha amevaa gauni na kiremba kichwani.hipukizi huyo asiyeishiwa vituko amedai kuwa, anamkubali sana Alikiba hivyo alipomuona wiki iliyopita katika kipindi cha Lip Sync Africa kinachoruka kupitia runinga ya MTV SA akiwa amevalia mavazi kama hayo wakati alipokuwa akiimba wimbo wa ‘Vulindlela’ wa Brenda Fassie.

“Unajua mimi namkubali sana Alikiba, hivyo nilivyoona amefanya kitu kile na mimi nikasema ngoja nifanye kama ‘Cover’ ila sikuvaa gauni la bosi wangu wala sikuvaa gauni. Mimi naona niliva mavazi ya kawaida tu, labda nyinyi ndiyo mnaona gauni lakini kwangu mimi ile ni nguo tu ya kawaida,” Harmo amekiambia kipindi cha E News cha EATV.
Kwa sasa rapper huyo anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Nundu’ ambao amemshirikisha Cpwaa na Ronei.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment