Hii ndio barua ya Diamond kwa wasanii wa Bongo Flava

Diamond Platnumz ameamua kuwapa wasanii wenzake somo zito kuhusu muziki wao na malengo ya kufika mbali

Kupitia mtandao wa Instagram, hitmaker wa ‘Marry You’ ameandika:
Leo ningependa nitoe ujumbe huu kwa wasanii wenzangu pendwa… Siku hizi mjini kila mtu anajifanya yeye soko la Muziki analijua sana na bingwa wa kuelekeza na kukosoa nyimbo za watu….Pasipo kujua kuwa kila nyimbo ina soko lake na kila mwanamuziki anapotoa nyimbo anakuwa na malengo ama plan ambayo ameidhamiria…leo ntakupostia baadhi ya nyimbo ambazo wakati nazitoa zilidharauliwa, zilipingwa sana na wanaojifanya wajuaji wa Muziki… pasipo kujua kuwa dhamira ama nini yalikuwa malengo yangu….kwakuwa nilikuwa na imani na kufahamu nikifanyacho basi nikawa nawaekea tu neno #MALENGO na leo hii nyimbo hizo ndio sababu kubwa ya mimi kuwa na Show za nchi ambazo kiukweli sijawai tegemea fika na kufanya show za Uwanjani….. sababu yangu kubwa leo ni kuwasihi wasanii wenzangu kuwa mnapokuwa na kitu ambacho mnamalengo ama target nacho msiogope kukisimamia…lakini pia kuwajuza kuwa kila kanda ina maadhi ya muziki wake ambao unaupenda, hivyo ukitaka kufanikiwa kushika kanda zote usiogope kufanya Muziki tofautitofauti ili kuongeza Mashabiki ila ukiogopa kufanya muziki wa mahadhi flani kisa wabongo wataongea na kuamua tu kutoa kina “UKIMUONA” Basi hatutafanikiwa kuteka Masoko na chi zingine… #SimbaInZambia
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment