Kama wewe ni mzazi ujumbe huu wa Ray C lazima ukutoe machoziMsanii wa muziki wa Bongo Fleva,Ray C ametumia vizuri siku ya leo ya akina Mama Duniani kwa kuwakumbuka Wazazi wa watoto watatu walionusurika kwenye ajali ya Gari huko Karatu mkoani Arusha kwa kuwapa ujumbe wa faraja wenye maneno ya kutia Moyo.

Watoto watatu walionusurika na ajali ya Basi ya Karatu Mapema leo wakisafirishwa kwenda Marekani kwa Matibabu

Ray C amesema Mungu yupo mbele ya watoto hao na kwavile wameondoka wakiwa wanahema basi watarudi wakiwa wanahema na wenye Afya.

“Mtapona kwa nguvu ya Mungu kupitia madaktari….na mtarudi salama…Ya Mungu ni mengi na tayari kashawaonyesha kupitia mliyopitia na bado mnahema“Ameandika Ray C .

Ray C pia aliwapa moyo akina mama wa watoto hao watatu ukizingatia leo ni siku ya Akina Mama duniani kwa kusema waendelee kuomba na kumuamini Mungu kwani yeye ndiye ngao pekee iliyobakia kwenye maisha yao.

“Happy Mother’s day kwa wamama wote Wa hawa watoto,Mungu azidi kuwaonyesha uwepo wake kwenu muda wote na mzidi kumuamini kuwa yeye ndio ngao ya Maisha yenu“Ameandika Ray C kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Wazazi wa watoto hao watatu majeruhi wa ajali ya Basi ya Karatu iliyoua watu 35, wameondoka leo asubuhi hapa nchini kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya Matibabu zaidi .

By Godfrey Mgallah

 
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment