Kourtney Kardashian athibitisha mahusiano yake na Younes Bendjima

Kourtney Kardashian amethibitisha kutoka kimapenzi na Younes Bendjima, huku akimrushia matusi baba wa watoto wake na mpenzi wake wa zamani Scott Disick.


Chanzo cha karibu na mwanamama huyo kimesema kuwa Kourtney kweli anatoka kimapenzi na Younes ila uhusiano wao haupo serious sana kwa upande wa Kourtney , yeye ana enjoy maisha tu, na ndio maana anaonekana nae kila muda.

Kourtney Kardashian kwa sasa ameamua kutupilia mbali mahaba yake kwa Scott Disick, na kuhamishia kwa kijana Younes mwenye miaka 23 ambaye mpaka sasa bado hajakutana na watoto wa Kourney aliozaa na Scott amabao ni Mason- 7, Penelope-4, na Reign -2.
Kama umewahi kuangalia kipindi cha Keeping Up with the Kardashians, utaona jinsi Scott anavyoonesha kulihitaji upya penzi la Kourtney wakati huo bi dada akihamisha mahaba na kuyapeleka upande mwingine.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment