Kumnadi Lowassa ulikuwa mzigo mzito- Pro. Lipumba

Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Pro. Ibrahim Lipumba amesema kuwa ameamua kurudi CUF kutokana na mkanganyiko uliokuwepo UKAWA, baada ya kumchagua Lowassa kugombea nafasi ya Urais huku akisema kumnadi kiongozi huyo ulikuwa mzigo mzito.

Pro.Lipumba ameyazungumza hayo katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv huku akisema kuwa Mh. James Mbatia ndiye aliyemuunganisha na Lowassa.
Akizungumzia kuhusu kumpokea na kumtambulisha kwa viongozi wa UKAWA aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa wakati anatoka CCM, Prof. Lipumba alisema: “Mbatia ndiye aliyeniunganisha na Lowassa. Sikuwa na namba zake, na wakati anakuja, nilisema wazi suala la rushwa ni mfumo siyo mtu.Mzigo mzito anapewa Mnyamwezi, lakini huu wa kumnadi Edward Lowassa ulinizidi uzito, nisingeweza kuubeba.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment