Kuwa baba imenifanya kupunguza ‘totozi’ – Diamond

Msanii Diamond Platnumz amefunguka na kusema kwamba tangu alipoanza maisha ya kifamilia na kuwa baba kumemfanya kuzidi kuwa makini na kupunguza kuwa na mahusiano ya kimapenzi yasiyoeleweka.

Akizungumza katika kipindi cha The Trend kilichorushwa na NTV mwishoni mwa Weekend hii, Diamond amesema jambo la kuwa na watoto limemfanya kuzidi kupambana ili aweze kuwatengezea watoto wake maisha mazuri ili baadaye na wao wajivunie kuwa kuna mtu alikuwa akiwapigania.
“Kuwa baba imenifanya kuwa makini zaidi, nifanye kazi kwa juhudi na niwe nazingatia, imenifanya hata nipunguze totozi kidogo, imenifanya nitulie kwa sababu unajua nina watoto halafu wananitengemea nikiwa kama mzazi lazima niwatengenezee future nzuri kwa maisha ya baadae ili kesho na kesho kutwa waseme tulikuwa na baba yetu akatuwekea misingi,”amesema na kuongeza.
“Pengine ndio imenipa akili ya kufungua Record Label na vitu tofauti tofauti, namshukuru mzazi mwenzangu namshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kunipa watoto na ninawapenda sana,” ameeleza Diamond.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment