Majeruhi kutibiwa bila PF3 – Waziri Nchemba

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema kuwa majeruhi na mahututi asiyeweza kutoroka na mtu mwenye majeraha yasio na utata wapewe matibabu kwanza bila PF3.

Waziri Nchemba ameyaanisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagramu hivi:
Tumeamua, majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka,na mtu mwenye majeraha yasiyo na utata wapewe matibabu KWANZA bila PF3.
Hatua za kufuata PF3 zianze mara moja wakati akiendelea kupewa matibabu, hii tunalenga kuokoa maisha yao kwanza.

Utaratibu huu unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vyetu vya usalama ili kubaini ukweli jeraha la mhusika.
WMNN -Hon. Mwigulu Nchemba.
18/05/2017
Dodoma-Tanzania


Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment