Majeruhi watatu wa ajali ya Basi Karatu wawasili salama Marekani

Majeruhi watatu wa ajali ya basi iliyotokea huko Karatu wiki mbili zilizopita wamewasili nchini Marekani salama walikoenda kwa ajili ya Matibabu zaidi .

Mapema jana watoto watatu majeruhi wakipelekwa KIA kwa ajili ya kuanza safari
Akithibitisha taarifa hizo Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amesema  Ndege iliyochua watoto hao majeruhi kutoka uwanja wa KIA jana asubuhi  imewasili Mjini Charlotte NC, nchini Marekani saa Moja iliyopita.
Watoto hao wamepelekwa Moja kwa Moja hospital kuu mjini Charlotte kwa ajili ya kuimarishwa kiafya (medical stabilisation), na baadae watachukuliwa kwa ndege nyingine maalumu (air ambulance) kuelekea hospitali ya Mercy, Iliyopo Sioux City, katika Jimbo la Iowa kwa huduma kamili za matibabu.
Ndege iliyochua watoto wetu KIA jana imewasili Mjini Charlotte NC, nchini Marekani saa Moja iliyopita (majira ya saa 3 asubuhi, saa za Afrika ya Mashariki). Watoto wamepelekwa Moja kwa Moja hospital kuu mjini Charlotte kwa ajili ya kuimarishwa kiafya (medical stabilisation), na baadae watachukuliwa kwa ndege nyingine maalumu (air ambulance) kuelekea hospitali ya Mercy, Iliyopo Sioux City, katika Jimbo la Iowa kwa huduma kamili za matibabu“Ameandika Lazaro Nyalandu kwenye kurasa zake za mitandao ya Kijamii.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment