Mama yake Halima Mdee alinipigia simu – Spika Ndugai

Baada ya Halima Mdee kuombewa msamaha na wabunge na kusamehewa, Spika wa bunge, Job Ndugai, amesema kwamba mama wa mbunge huyo alimpigia simu akitaka kumuona spika.

Wiki kadhaa zilizopita, Halima Mdee alitumia lugha hizo bungeni. Ambapo Spika Ndugai ameliambia bunge hilo kuwa, dawa ya mtu akikukosea kosa kubwa ni kumsamehe.
“Sisi Waafrika bado tuna changamoto kubwa sana ya kutokujifunza kuheshimiana, yani sisi tunadharauliana sana kupita kiasi. Sijui ni Mila sijui ni desturi sijui ni nini, mama yake Halima alinipigia simu mara kadhaa alitaka kuja kuniona, nikamwambia wala hakuna neno mama tutayamaliza wenyewe, lakini nikamwambia na wewe kosa lako pia malezi inaelekea kuna mahali hukutimiza wajibu wako vizuri, lakini pia huwezi kumlaumu mama moja kwa moja wakati mwingine watoto wanajifunza barabarani huko kuwa na tabia za ajabu maana sisi wote wazazi, maana yake si lazima awe spika awe nani kwa neno alilolisema Halima humu ndani, Kamati ikaenda kuchukua kamusi kwa neno lile alilosema,” alisema Spika Ndugai.
“Kwa maana yake mtu huyo unaemwambia ‘fala’ ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri, ni mtu mpumbavu, ni mtu bwege, ni mtu mjinga, ni mtu bozi, ni gulagula ndiyo maana nikasema sisi Waafrika hata kama humpendi kwa namna gani mwenzako, huwezi kumfanyia hivyo yani mradi tu yeye ni binadamu huwezi kumfikisha hapo sijui awe amekufanyaje labda unaweza ukasema namna hiyo, lakini vinginevyo you cant do that kwahiyo amestep yani over ni mtu ambaye kwa vyovyote vile kwa mtu wa kawaida lazima utampa adhabu lakini ni busara kubwa ya bunge hili na wote ambao mmezungumza kwamba kwa mtu ambaye amefanya makosa makubwa namna hii kwa kweli adhabu yake ni kusamehewa hiyo ndiyo adhabu yake haswa.”
Aprili 14 mwaka huu Halima Mdee alitoa lugha chafu bungeni katika uchaguzi wa bunge la Afrika Mashariki na kupelekea kuitwa na kamati ya maadili na baadaye kusamehewa.
Na Emmy Mwaipopo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment