MAN WALTER AELEZEA KILICHOMKWAMISHA KUMRUDISHA 20 PERCENT

Mtayarishaji wa muziki Bongo Flava, Man Water amezungumzia kazi za 20 Percent ambaye yupo chini ya usimamizi wake pamoja na ukimya wake. Mshindi huyo wa tuzo kibao ameiambia Dizzim Online kuwa kuna vitu vilikuwa vinaendelea kwa 20% ambavyo vilisababisha mambo mengi kutokea ikiwemo na ukimya wake.

“Unajua kuna jamaa walikuja kutaka kumsimamia 20% akanishirikisha nikamwambia hao jamaa inabidi watokee kwangu ili niweze kuwakabidhi nyimbo alizofanya na kuwaelekeza nini cha kufanya. Lakini nafikiri ni watu ambao walitaka kujaribu, sidhani kama wanauwelewa muziki vizuri, so bado nipo naye mwenyewe na jambo hilo limetokea bado nipo naye ingawa limesababisha spidi kupungua kwasababu sisi tulikuwa tunawasikiliza wao,” amesema.
Man Walter alimsaidia kwa kiasi kikubwa Percent kufahamika ikiwa pamoja na kushinda takriban tuzo tano za KTMA enzi muziki wake upo juu.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment