Mimi na Diamond tuna mahusiano zaidi ya kimapenzi – Jackline Wolper

Muigizaji Jackline Wolper amesema yeye na msanii Diamond Platnumz wana uhusiano wao ambao ni kiwango cha juu kwani wamekuwa wakishirikiana katika mambo mengi.

Jackline Wolper
Katika segment ya kikaongoni inayorushwa na EATV (facebook) inayotoa fursa kwa watu kumuuliza mgeni maswali, moja ya swali lilitaka kujua ni iwapo Wolper alishakuwa na uhusiano wa kimapenzi na Alikiba, Jux, Ray Kigosi na Diamond Platnumz.
“Alikiba ndiyo, Jux alikuwa rafiki yangu wa karibu, Ray Kigosi yule ni kaka yangu namuheshimu sana, Diamond tuna mahusiano zaidi ya kimapenzi, yaani kikazi.
“Diamond tuna mahusiano mengi sana zaidi hata ya kimapenzi, ni bosi wangu, rafiki yangu, mshauri wangu, yaani na mahusiano nae mengi, umenielewa?, kikazi na vitu vingi,” amejibu Wolper.
Katika hatua nyingine muugizaji huyo amesema kinachomzuia kufanya movie na wasanii wa nje ni kutojua kingereza kwa ufasaha zaidi kitu ambacho ameanza kukifanyia kazi.
“Na wish kufanya hivyo lakini kidogo lugha gongano, ndio maana kuna mwalimu wangu huwa anakujaa kila saa 10 pale ofisini kwa hiyo sasa hivi kidogo naprove, kujua lugha kikweli hiyo ndio dream yangu sana kwa sababu kuna wasanii wa nje nawapenda na ninaamini naweza kufanya nao kazi, kwa hiyo nikiwa kwenye zile level zile za juu nitafanya,” ameleeza Wolper.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.