Mkubwa na Wanawe hawamsaidii msanii anayefanya kazi binafsi – Aslay

Msanii kutoka kundi la Yamoto Band, Aslay amefunguka kuwa, Mkubwa na Wanawe hawatoi support kwa msanii anayefanya kazi binafsi (Solo Artist).

Kupitia kipind cha Zero Planet cha Ice Fm mkoani Njombe, hitmaker huyo wa ‘Angekuona’ aliulizwa juu ya kauli aliyoitoa Beka One, ambaye na yeye ni member wa kundi hilo kinachoongozwa na Said Fella aka Mkubwa Fella.
“Ni kweli Mkubwa yeye anasimamia Yamoto Band, Mkubwa hasimamii msanii mmoja mmoja, kwahiyo unatakiwa ufanye kitu cha ziada ilimradi ngoma zako zifike. Wenzangu wanaandaa vitu vinakuja lakini mimi nimefanya kama nimewahi kuwaonesha njia,” amesema muimbaji huyo.
Kwa sasa Aslay ameachia wimbo wake mpya ‘Usiitie Doa’, aliomshirikisha malkia wa muziki wa taarab nchini Khadija Kopa.
Imeandikwa na: @gamideetz
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment