Moni asimulia kilichotokea walipotekwa wakiwa na Roma

Moni Centrozone amesimulia kilichotokea katika tukio la utekaji walilofanyiwa mapema mwezi April mwaka huu akiwa pamoja na Roma, producer Bin Laden na Imma wakiwa katika studio za Tongwe Records.

Rapper huyo amesema, siku ya tukio kuna mtu alimuita Roma nje akihitaji simu yake [Roma] huku wakilazimisha ampigie J-Murder, kisha wakachukua simu na kuanza kutumia maneno ya ulaghai ya kuwa walitaka huduma ya studio kama wasanii.
“Yule jamaa wakati ananiambia nimpe simu ya Roma, wakati naifata simu ya Roma akawa ameshaingia akaiwahi, akaichukua akaniambia wewe ndo Moni? Wewe ndio sembe sembe dona? Kaa hapo chini nimekwambia, kaa kwenye kochi simu yako iko wapi? Nikamwambia simu yangu ipo kwenye chaji, akamuuliza na Bin Laden, naye Bin Laden akatoa simu. Akauliza Junior yuko wapi? Mpigie J-Murder sasa ile hali ya vitisho ikawa imeshaanza,” amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Kumpigia J-Murder hata kabla sijamaliza maelezo yaani ile bosi kuna watu wamekuja hapa studio, jamaa akanipora simu. Oya inakuwaje J-Murder, sisi hapa tunataka kurecord, tunataka kurecord nyimbo sita,” ameongeza.
Rapper huyo ambaye kwa sasa ameachia wimbo mpya, ‘Tunaishi Nao’ samesisitiza, “Muda ambao nakumbuka nimesali sala zangu za mwisho ni ule pale, nikaona dah basi kama kuna kitu nimefanya au kuna kitu nimekosea basi ni kumuachia Mungu.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment