Mose Iyobo ‘amchimba biti’ Aunt Ezekiel kulala kambi

Ni kawaida kwa wasanii movie kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya kushoot filamu zao, sasa mpenzi wa malkia wa filamu Aunt Ezekiel,  Mose Iyobo amempiga marufuku mrembo huyo kulala kambini kisa wivu wa kimapenzi.

Aunt Ezekiel, Cookie na Mose Iyobo
Mose Iyobo ameimbia show ya XXL kuwa mwanzoni suala hilo lilikuwa linamuumiza kwa sababu walikuwa wanakutana mara chache sana.
“Lakini tulipokubaliana yeye ni Mama na mimi ni Baba vitu vya kambini vikaisha, kama ni kushoot hakikisha unarudi nyumbani sio kulala huko huko. Nyumba ipo ukalale kambini kwa kisingizio gani  na haushoot alfajiri, bali ni mchana kwa nini usilale nyumbani uamke asubuhi ndio uende,  mimi sitaki mambo ya kulala kambini, basi alinielewa tu… ni vivu wa mapenzi na wasiwasi siunajua ndio akili,” ameeleza Mose Iyobo.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment