Mtu wangu wa nguvu ni Diamond sio Alikiba – Shilole

Msanii wa muziki, Zuwena Mohammed aka ‘Shilole’, amedai yeye ni shabiki wa damu wa Diamond na sio Alikiba

Akiongea katika Kikaango cha EATV Jumatano hii, Shilole amedai anampenda Diamond kutokana na vile alivyo pamoja na vitu anavyofanya.
“Mimi namkubali zaidi Diamond Platnumz kuliko Alikiba,” alisema Shilole. “Nampenda Diamond kutokana na mambo yake na vile alivyo, kwa hiyo kila mtu ana watu anaowakubali na kuwapenda,”
Katika hatua nyingine Shilole amedai yeye alishtuka mapema na kuchomoka kwenye tasnia ya Bongo Movie maana kama aliona kuwa mbele itakuja kuyumba.
Alisema yeye ameridhika na muziki kwani muziki unamlipa na umempa mafanikio makubwa ambayo kama angekuwa kwenye filamu huenda asingeyapata
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment