MZEE YUSUF ALITAKA AIFUTE JAHAZI MODERN TAARAB BASATA WAKAMZUIA

Baada ya kuacha kufanya muziki, Mzee Yusuf alitaka kuifuta kabisa Jahazi Modern Taarab, lakini Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA lilimzuia.

Amesema kwa mujibu wa sheria za serikali, haiwezekani tu kuifuta bendi kwakuwa inaweza kuendelezwa na watu waliosalia. “Nilikusudia niivunje Jahazi kama ninavyovunja nyumba,” Mzee Yusuf alikiambia kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM. “Lakini sheria za nchi hakuna utaratibu huo, wewe ondoka na ujiachishe kila kitu.”
Aliongeza kuwa kwa sasa hajui chochote kinachooendelea kwenye bendi hiyo na wala hataki kujua. Hata hivyo alikiri kuwa tangu ameacha muziki ameyumba kiuchumi japo hajutii na moyo wake una amani.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment