Niombeeni nipate mume bora, mimi na Diamond… – Wema

Msanii wa filamu, Wema Sepetu amewataka mashabiki wake kumuombea apate mume bora atakayekuwa na heshima na wala asiwe mtu maarufu na siyo kumhusisha kila mara na uhusiano wa kimapenzi na msanii Diamond Platnumz.

Amesema hayo wakati akimjibu shabiki katika kurasa wake wa Instagram, na kumtaka atambue Diamond ni baba wa watoto wawili kwa sasa na ifike kipindi watu waamini kwamba hakuna kinachoendelea kati yao.


“Sasa baby aliokwambia namtaka Damond ni nani? Life has to go on, yule ni baba wa watoto wawili jamani. Its about time u guys accept that me and Naseeb no more. Mnachotakiwa kuniombea ni nipate mwanaume bora na siyo bora mwanaume na mwenye heshima zake,” aliandika Wema Sepetu Instagram.

Malkia huyo wa filamu hivi karibuni alikutana na Diamond katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Sallam na kupiga picha ambazo zilizua gumzo huko mitandaoni.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment