Nitaenda Uganda kwa ajili ya mazishi ya Ivan – Diamond

Diamond athibitisha kuwa atahudhuria katika mazishi ya Ivan Ssemwanga ambaye alikuwa mzazi mwenzake na Zari The Bosslady
Muimbaji huyo amesema hayo mbele ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Nairobi, katika kipindi cha The Trend kilichokuwa kinaruka moja kwa moja kupitia runinga ya NTV.

“Kiukweli umekuwa wakati mgumu na mpaka sasa umekuwa wakati mgumu, nilikuwa nipo booked muda kidogo kuhusiana na msiba umetokea, sasa kucancel to ghafla show ya watu unajua inawezekana ukapata twasira tofauti, wengine wakachukulia tofauti sikuwa na jinsi.Lakini niliongea na mzazi mwenzangu akanielewa lakini nikimaliza hapa show nitaenda Uganda kwa sababu ya mazishi na baada ya hapo ndio nitarudi nyumbani,” amesema Diamond
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment