Ray C afunguka kuhusu hali ya urafiki wa na Lady Jaydee

Ray C amefunguka kuhusu mahusiano yake na Lady Jaydee kwa sasa baada ya kuonekana wakiwa kwenye picha ya pamoja waliopiga April mwaka jana walipokutana baada ya kutoonana kwa miaka mingi.

Muimbaji huyo wa Unanimaliza, amekiambia kipindi cha Vmix cha Channel Ten, hana mawasiliano na Jaydee na ni muda mrefu hawajawasiliana.
“Mimi na Lady Jaydee hatuwasiliani wala hatuna ukaribu, it’s been long time hatujawasiliana ila nakumbuka last year alinipigia simu na kuanzia hapo hatujawahi kuwasiliana,” amesema
Ray C.
Picha waliyopiga Lady Jaydee na Ray C mwaka jana walipoonana
“Kitu ambacho watu hawafahamu kuhusu mimi na Jide ni kwamba tulikuwa label moja wote ambayo ni Smooth Vibez na albamu ya Jide ndio ilikuwa ya kwanza kutoka then nikatolewa mimi. So jide ni mtu ambaye tumefanya kazi sehemu moja kwenye Radio, kwa hiyo mimi na Jaydee ni kama familia tu,” ameongeza.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment