Serikali ibadili jina shindano la Miss Tanzania – Afande Sele

Baadhi ya wadau akiwemo msanii mkongwe wa muziki nchini kutoka Morogoro, Afande Sele ameonyesha kutoridhishwa na zawadi ya gari aliyopewa Miss Tanzania 2016/17, Diana Edward kwa madai limechakaa na linashusha hadhi ya mashindano hayo nchini.


Afande Sele
Rapa huyo ameishauri wizara husika kubadili jina la shindano hilo kwa madai wanalitia aibu Taifa.
“Utapeli ni nini?. Gari ya Miss Tanzania 2017 na gari ya Miss Tanzania 2011 zinatoa jibu la swali hilo,” aliandika Afande Sele Intagram. “Lakini pia ni vyema tukamuomba waziri husika katika masuala hayo akamuulize muandaaji wa Miss Tanzania kama ni kweli ameamua kuzeeka labda hata kufa na shindano lake?,”
Aliongeza, “Na kama kweli iko hivyo basi itoshe pia kubadili jina la shindano kwa kuliita miss jina lake badala ya kuendelea kutia aibu faifa kwa kuliita Miss Tanzania huku likikosa hadhi ya kitaifa katika maeneo yote kwa makusudi na maslahi yake yeye mtu mmoja tu. Aibu yake aibu yetu. Imetosha sasa, imetosha sana,”
Miss huyo alikabidhiwa gari hilo week iliyopita baada ya kuzungushwa kwa zaidi ya miezi sita.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment